Wanaume: Mambo 7 ya kuzingatia kabla ya ‘kuzama DM’

HomeElimu

Wanaume: Mambo 7 ya kuzingatia kabla ya ‘kuzama DM’

‘Kuzama’ au ‘Kuslide DM’ ni lugha iliyozoeleka mtandaoni. Hicho ni kitendo kutuma ujumbe moja kwa moja kwa mtu kwenye mitandao ya kijamii, katika uwanja ambao hausomwi na watu wengine (Direct Message au ‘DM).

Unaweza kuvutiwa na mtu kupitia mtandao, lakini kwa kuwa hufahamiani na mtu huyo katika maisha ya kawaida inakuwa ngumu kumtumia ujumbe na kuweza kufahamiana na yeye.

Hizi ni njia 10 ambazo zinaweza kurahisisha zoezi la ‘kuslide DM’ hususan kwa wanaume au wavulana wanaotafuta wenza kupitia mtandao.

1. Mstari wa kwanza ndio kila kitu.

Salaam unayoanza nayo unapomtafuta mtu ambaye hufahamiani naye mtandaaoni, ina nafasi kubwa kufanya mtu huyo aamue iwapo anataka kuendelea kuwasiliana na wewe au aamue kukukalia kimya kabisa (kukupotezea)

Usifanye makosa ya kumuita majina ya kimapenzi au majina mengine ambayo unafahamu kwamba utakuwa unacheza pata potea. Tumia maneno ya kawaida yenye kuonesha uungwana ili yakupe fursa ya kupokelewa.

2. Usitumie majina (User Name) zisizoeleweka

Epuka kabisa majina ya kihuni au kihalifu. Itamtisha mtu unayejaribu kufahamiana naye.

3. Maudhui ya ukurasa wako

Utakapomtumia ujumbe kupitia ‘DM’, jambo la kwanza atakalolifanya ni kuangalia jina lako na kwenda kwenye ‘post’ zako ili aone maudhui unayopendelea.

Hivyo kabla ya ‘kuslide DM’ hakikisha kwanza picha ulizopost na ‘caption’ zake hazitii shaka.

4. Nenda moja kwa moja kwenye lengo lako

Kitendo cha kupokea ujumbe kutoka kwa mtu usiyemfahamu kinaweza kuzua mashaka, mashaka yataongezeka iwapo mtu huyo haeleweki anataka nini.

Epuka ‘siasa nyingi’, usizunguke, nenda moja kwa moja. Mfano “Habari, naitwa Juma Jacob. Je tunaweza kufahamiana?”

5. Epuka kuandika maneno kwa kifupi.

Usiandike ‘VP’ badala ya ‘vipi’, usiandike ‘ktk’ badala ya ‘katika’. Achana kabisa na ufupisho wa maneno ambao mara nyingi hufanywa na wanafunzi wa sekondari.

6. Epuka masuala ya kidini na kikabila.

Inawezekana wewe umeishika sana dini yako, lakini hiyo haikupi uhalali wa kutaka au kuamini kwamba na unayejaribu kumfahamu anaamini katika njia zako. Epuka maneno ya kidini.

Pia usiingie kwenye mtego wa kuleta mijadala ya ukabila, baki kwenye mambo ambayo sehemu kubwa ya jamii inaweza kukubaliana

7. Kuwa na kiasi

Usiwe na maneno mengi kupita kiasi, kuwa makini sana usionekane kama muigizaji tu ambaye sio mkweli

error: Content is protected !!