Wanawake 20 waliowahi ‘kutoka kimapenzi’ na Rick Rosss

HomeMakala

Wanawake 20 waliowahi ‘kutoka kimapenzi’ na Rick Rosss

William Leonard Roberts (II) aliyezaliwa Januari 28, 1976, ni mwanamuziki kutoka nchini Marekani anayefahamika kama Rick Ross. Rick Ross pia ni mmiliki wa ‘label’ ya Maybach Music Group.

Rick Ross ambaye alikuja Tanzania mwaka 2012 kwenye tamasha la muziki la Fiesta, amewahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanawake kadha wa kadha, jambo wengine zilibaki kama tetesi ambazo haziuthibitika.

Wanawake 20 walioko kwenye ‘historia ya kimapenzi’ ya Rick Ross ni hawa hapa.

1. Keyshia Dior

Ni mwanamitindo kutoka Jamaica aliyekuwa mpenzi wa Rick Ross mwaka 2014

2.Lila Galore

Mwanamitindo huyo kutoka nchini Marekani, alivalishwa pete ya uchumba na Rick Ross tarehe 17 Septemba 2015 lakini penzi lao lilivunjika mwezi Desemba 2015.

3. Khloe Kardashian

Machi 2014 kulikuwa na tetesi kwamba Rick Ross ‘ametoka’ na mwanahabari huyo ambaye ni ndugu wa aliyekuwa mke wa Kanye West, Kim Kardashian.

4. Briana Camille

Ni mwalimu wa mazoezi ambaye alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Rick Ross kwa muda mrefu. Walipata watoto wawili, msichana Berkeley Hermes na mvulana Billion Leonard Roberts.

5. Paige Imani

Rick Ross na wanamitindo ni chanda na pete, Paige ni mwanamitindo mwingine ambaye aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Rick Ross. Paige na Ross walidumu kwenye penzi kuanzia  Januari hadi Octoba 2014.

6. Alexis Sky

Binti huyo aliyezaliwa Julai 14 2014, ni mwanahabari, mjasiriamali, muigizaji na mwanamitindo. Aliwahi ‘kutoka’ na Rick Ross.

7. Foxy Brown

Alikuwa mpenzi wa Rick Ross mwaka 2008.

8. Liz Hagelthorn

‘alidate’ na Rick Ross mwaka 2017.

9. India Westbrook

Ni mwanamitindo ambaye alikuwa mpenzi wa Rick Ross kuanzia Oktoba 2016 hadi Aprili 2017.

10. Chandra Davis

Ni muigizaji raia wa Marekani, alikuwa kwenye mahusiano na Rick Ross mwaka 2016.

11. Briteady

Naye ni mwanamitindo, alikuwa mpenzi wa Rick Ross mwezi Mei hadi Novemba 2016.

12. Skrawberry

 

Ni mcheza muziki (Dancer) ambaye alikuwa mpenzi wa Rick Ross mwaka 2015.

13. Lastonia Leviston

Msichana huyu ambaye aliwahi kulipwa fidia ya dola milioni tano za Kimarekani na mwanamuziki 50 Cent baada ya kuvujisha video zake za faragha, aliwahi kuwa mpenzi wa Rick Ross (2000 -2002)

14. Ming Lee

Mfanyabiashara huyo alidumu kwenye penzi na Rick Ross kuanzia Novemba 2014 hadi Februari 2015.

15. Premadonna

Huyu ni mwanamuziki wa nchini Marekani ambaye mwaka 2013 alikuwa kwenye ‘penzi’ na Rick Ross

16. Christelle Blanche

Ni mwanamitindo ambaye penzi lake na Rick Ross lilidumu kwa miaka miatatu (2011-2014)

17. Shateria Moragne-El

Mbunifu huyo wa mavazi alikuwa mpenzi wa Rick Ross wakati anakuja Tanzania mwaka 2012. Penzi lao lilianza 2009 na kufikia tamati 2013.

18. Tia Kemp

Huyu ndiye mwanamke alikaa kwenye mahusiano na Rick Ross kwa muda mrefu zaidi. Tanagu 2003 hadi 2015 walipoachana rasmi wakiwa na mtoto mmoja.

19. Elise Neal

Mwanamke huyo muigizaji kutoka Marekani ambaye amemzidi Rick Ross umri kwa miaka 10 (Elise amezaliwa mwaka 1966 wakati Rick amezaliwa mwaka 1976) alikuwa mpenzi wa Ross kati ya mwaka 2010 na 2011.

20. Hamisa Mobetto

Hamisa Mobetto ni mwanamitindo, mwanamuziki na mfanyabiashara kutoka Tanzania ambaye wiki iliyopita ameonekana akiwa na Rick Ross katika viwanja vya starehe. Video zao zinatuma ujumbe kwamba wapo katika mahusiano.

 

 

error: Content is protected !!