Mambo matano ya kuzingatia kwenye barua ya kuomba kazi

HomeMakala

Mambo matano ya kuzingatia kwenye barua ya kuomba kazi

Barua ya maombi ya ajira ina nafasi kubwa sana katika safari yako ya utafutaji. Uandishi mbaya wa barua unaweza kukosesha kazi ambayo una kila sifa za kuipata.

Pamoja na mambo mengine yanayohusiana na uandishi wa barua rasmi ya maombi ya ajira, ukizingatia mambo yafuatayo utaongeza uwezekano wa kuitwa kwenye usaili na hatimaye kupata kazi;

5. Jikite kwenye mahitaji ya muajiri

Barua ya kazi sio kwa ajili yako binafsi. Hakikisha unajikita kwenye kuonesha jinsi ambavyo ujuzi wako, mafanikio yako katika kazi na uzoefu wako vitamnufaisha muajiri atakapokupa kazi unayoiomba.

Epuka kabisa kutaja mambo ambayo yatakunufaisha wewe binafsi utakapopata kazi unayoomba. Barua inapaswa kumuonesha muajiri kwamba wewe ndiye mtu sahihi kuweza kufanikisha malengo ya kazi hiyo ambayo mara nyingi yanaonekana kwenye tangazo la ajira.

4. Onesha shauku (Enthusiasm)

Soma vizuri tangazo la ajira na utazame mambo yaliyokuvutia kwenye kazi kazi hiyo. Tumia maneno (mafupi) yatakayoonesha kwamba kazi hiyo imekuvutia hasa kwa namna ambavyo umekidhi vigezo vyote vinavyohitajika.

3. Barua iwe fupi

Licha ya maneno mengi unayoweza kuwa nayo kichwani kuonesha jinsi gani unastahili kupata kazi unayoiomba, epuka kuwakera watakayoisoma barua yako. Barua ya kazi sio mashairi ama riwaya, lazima iwe fupi.

Wataalam wengi wa masuala ya ajira duniani kote wanakubaliana kwamba barua ya maombi ya kazi haipaswi kuzidi ukurasa mmoja.

2. Weka mifano ya kazi

Inawezekana umewahi kufanya kazi zinazoendana na kazi unayoomba, kuzitaja kazi hizo kwenye barua yako inaweza kukuongezea nafasi ya kuajiriwa. Zingatia kwamba mifano hiyo lazima iwe ya kazi zinazoendana au kuhusiana moja kwa moja na kazi unayoomba.

1. Maliza barua yako vizuri

Unaweza kuanza vizuri sana, lakini mwisho wa barua yako ukawa tiketi yako ya kubwagwa  kwenye mchakato wa ajira.

Barua ya kuomba ajira lazima ifungwe kwa maneno yanayonesha kwamba unatarajia kuonana wale unaowaomba kazi ili muweze kujadiliana ana kwa ana. Ni vyema ukaeleza kuhusu upatikanaji wako kwa ajili ya usaili iwapo barua yako itaweza kumshawishi muajiri au waajiri kukuita kwa ajili ya hatua hiyo.

Usisahau kushukuru.

error: Content is protected !!