Warithi wa kina Mdee

HomeKitaifa

Warithi wa kina Mdee

Leo jijini Dar es Salaam, Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) linaketi kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yahusuyo chama hicho na mustakabali wa siasa.

Macho na masikio ya watu wengi yakisubiri uamuzi utakaochukuliwa na uongozi wa chama hicho kama kitawafukuza wabunge wa viti maalumu 19 au kuwabakiza.

Taarifa kutoka ndani ya Chadema zimedokeza kuwa kuna uwezekano wa chama hicho kupeleka majina mengine ya wabunge wa viti maalumu kuchukua nafasi za kina Mdee iwapo Baraza Kuu litabariki kufukuzwa kwao uanachama kulikofanywa na Kamati Kuu Novemba 27,2020.

Wabunge hao wa viti maalumu wanadaiwa kukiuka katiba na kanuni za chama hicho baada ya kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu Novemba, 24, 2022 bila chama hicho kuwapitisha na hivyo kuitwa wasaliti.

Aidha, taarifa zinasema kuwa tayari Chadema wanajiandaa kupeleka majina mengine Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo itapeleka bungeni majiba hayo kujaza nafasi zitakazoachwa wazi na kina Mdee.

Majina yanayotajwa kuwarithi ni pamoja na Catherine Ruge (Katibu Mkuu wa Bawacha), Sharifa Mohamed (Kaimu Mwenyekiti wa Bawacha), Suzan Kiwanga aliyegombea jimbo la Mlimba (Morogoro), Grace Kiwelu, Joyce Mukya, Suzan Lyimo, Devotha Minja(aligombea ubunge Morogoro Mjini).

Wengine ni Upendo Peneza, Lucy Owenya, Rose Moshi, Rhoda Kunchela, Gimbi Masaba, Rose Mayemba, Aisha Luja, Husna Said, Nice Gisunte, Moza Ally, Dorcas Francis, Ruth Molle, Pamela Massay na Lucy Magareli.

Vigezo vinavyotajwa kutumika katika kufanya uteuzi ni wale waliogombea ubunge katika majimboni kwenye uchaguzi mkuu wa 2020, ushiriki na kujitolea kwao katika shughuli za chama kwa nyakati tofauti, elimu, mgawanyo kikanda na mgawanyo kwenye mabaraza ambayo ni Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA), Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), na Baraza la Wazee la Chadema ( BAZECHA).

error: Content is protected !!