Wasifu mfupi wa Jaji Luvanda aliyejitoa kesi ya Mbowe

HomeKitaifa

Wasifu mfupi wa Jaji Luvanda aliyejitoa kesi ya Mbowe

Septemba 6, 2021 vichwa vya habari vilighubikwa na taarifa za jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya ugaidi inayowakabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu kujitoa kusikiliza kesi hiyo.

Jaji Luvanda alifikia hatua hiyo baada ya watuhumiwa wote wanne kwenye kesi hiyo kuieleza Mahakama Kuu kuwa hawana imani kama jaji huyo atatenda haki kwenye kesi inayowakabili.

Sehemu kubwa ya maisha ya jaji huyu haifahamiki kwa umma, kidogo kinachofahamika ni kuwa Aprili 20, 2018 aliteuliwa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Magufuli kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Kabla ya uteuzi huo alikuwa mjumbe wa menejimenti ya Mahakama ya Tanzania na aliwahi kuwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Kesi ya Mbowe sio ya kwanza maarufu kwake, kwani aliisikiliza kesi nyingine maarufu ya kusafirisha dawa za kulevya iliyokuwa inawakabili wanandoa, mmiliki wa Blogu ya 8020, Shamimu Mwasha na mumewe, Abdul Nsembo ambao walihukumiwa kufungo cha maisha jela.

error: Content is protected !!