Watu 48 waokolewa mafuriko Morogoro

HomeKitaifa

Watu 48 waokolewa mafuriko Morogoro

Watu 48 wameokolewa katika mafuriko na kuhifadhiwa ofisi ya Kata ya Kihonda, Manispaa ya Morogoro kupatiwa msaada wa dharura na serikali, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jana.

Akizungumza jana, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Morogoro, Emmanuel Ochieng, alisema kikosi hicho kiliokoa watu na mali zao waliokumbwa na mafuriko katika makazi yao.

Ochieng alisema walipata taarifa ya matukio mbalimbali hasa Kata ya Kihonda, hivyo walifanya kazi ya uokoaji na kuokoa watu 48.

“Watu waliopo katika maeneo hatarishi katika mkondo wa kupitisha maji watafute utaratibu zaidi kwa usalama wao” alisema.

Alitoa wito kwa waliochimba mashimo ya taka na karo ni hatari kwa wanafunzi, wazee na watoto, hivyo aliwataka kuyafukia haraka.

 

error: Content is protected !!