Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeonyesha laini za simu zinazotumiwa na watu kwa ajili ya mawasiliano zimefikia milioni 58.1 Septemba, 2022 kutoka milioni 56.2 Juni mwaka huu.
Katika laini hizo mikoa mitano iliyoongoza ni Dar es Salaam (milioni 9.7) Mwanza (milioni 3.7) Arusha (milioni 3.4) Mbeya (milioni 3.08) na Tabora (milioni 3,06).
Pamoja na takwimu hizo bado hakuna mtoa huduma ambaye amezidi asilimia 35 ya laini zote zilizosajiliwa.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari ambaye amesema pia kwamba watumiaji wa intaneti nchini wameongezeka.
“Watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka 29,169,958 Juni 2022 hadi 31,122,163 Septemba 2022 sawa na ongezeko la asilimia 6.7%” Dkt. Jabiri.