Wema Sepetu amkana Aristotee hadharani

HomeBurudani

Wema Sepetu amkana Aristotee hadharani

Muigizaji kutoka nchini Tanzania, Wema Sepetu amekataa kumuongelea mfanyabiashara Aristotee na kusema kuwa hana faida kwenye maisha yake hivyo hawezi kuongea chochote kumuhusu yeye.

Alisema hayo alivyokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye hafla ya kutambulishwa kuwa balozi wa taulo za kike aina ya SuperMate maeneo ya Mikocheni, jijini Dar Es Salaam.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by ✨Wema App✨ (@wemasepetu)

“Kwanza kabisa nisingependa kumuongelea huyu mtu, yani nisingependa kabisa kumumpa airtime, sana sana nikiwa niko hapa , i just signed my deal alafu niendelee kumuongelea mtu ambaye hana maana hana faida kwenye maisha yangu,” alisema Wema.

Ikumbukwe Aristotee hivi karibuni alimsema Wema kwenye moja ya mahojiano na muandishi mmoja kwamba nyota huyo wa filamu nchini hana gari wala pesa huku akimfananisha na muigizaji mwingine Irene Uwoya.

error: Content is protected !!