Wimbo wa taifa kufanyiwa marekebisho

HomeKitaifa

Wimbo wa taifa kufanyiwa marekebisho

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yakubu Said, Mei 10, 2022 Dodoma amekutana na wataalamu wa Ala za Muziki  wakiongozwa na Mwalimu Mstaafu  Alexander Ngonyani  ambao wanapitia Wimbo wa Taifa, kwa ajili ya kubaini makosa yanayofanyika katika uimbaji na kuyarekebisha ili uimbwe kwa usahihi.

Wakiongozwa na Mwalimu Mstaafu wa Shule za Sekondari  Alexander Ngonyani wamepitia Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Uzalendo na Wimbo wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kubaini makosa yanayofanyika wakati wa uimbaji na hatimaye  kuyarekebisha ili nyimbo hizo ziimbwe kwa usahihi.

Wataalamu wakijadili makosa kwenye wimbo wa taifa, wimbo wa uzalendo na wimbo wa Afrika Mashariki

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Yakubu amesema kuwa Wimbo wa Taifa ni miongoni mwa Tunu za Taifa, hivyo unapaswa kuheshimiwa.

“Nawasisitiza kubainisha makosa yaliyopo kwenye nyimbo hizo, pamoja na usahihi unaotakiwa ili sisi kama Serikali tuchukue hatua ikiwemo kutoa elimu Kwa jamii ili makosa hayo yasirudiwe,” amesema Bw.Yakubu.

Nchi zenye nyimbo za taifa zinazofanana

Mzee Ngonyani amesema kuwa  chimbuko la kazi hiyo ni kutokana na kubaini makosa mengi katika uimbaji wa nyimbo hizo  unaofanywa na Taasisi, Shule na katika hafla mbalimbali za kitaifa, na tayari ameshawasiliana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na BASATA  ambao wamepokea utafiti huo ambao na kushauri aonane na uongozi wa Wizara ili kufanyiwa kazi ipasavyo.

 

 

 

 

error: Content is protected !!