Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kupitia Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar imelaani kitendo cha Watalii wawili wa jinsi moja (wanaume) kuvalishana pete wakiwa katika fukwe ya Hoteli iliyopo Jambiana Mkoa wa Kusini Unguja.
Taarifa zinasema uchunguzi unaendelea na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote walioandaa, kusimamia na kuhusika na tukio hilo ambalo ni kinyume na maadili na utamaduni wa Kizanzibari.
Kamisheni ya Utalii imesomeka ” “Mnamo September 20, 2022 Serikali ya Zanzibar ilipokea taarifa kuhusu tukio hilo baada ya video kusambazwa kwenye mitandao ya kijami, kilichotokea ni ukiukwaji wa sheria za Zanzibar, tunawahimiza Wawekezaji, Wadau na Wageni kutoshiriki kitendo chochote ambacho kinaweza kusababisha mmomonyoko wa maadili au kuvuruga amani katika Jamii zetu”
“Tunatoa onyo kwamba vitendo kama hivyo havitovumiliwa, kilichofanyika ni kinyume na sheria mbalimbali za Zanzibar ikiwemo sheria ya utalii ya Znz namba 6 ya mwaka 2009 kifungu cha 27 (2), tunaomba Wananchi wawe watulivu wakati Vyombo husika vikiendelea na hatua stahiki” imeeleza taarifa hiyo.