Yanga kuwakosa nyota wake watatu kwenye michuano ya kimataifa

HomeMichezo

Yanga kuwakosa nyota wake watatu kwenye michuano ya kimataifa

 

Klabu ya Yanga imethibitisha kwamba itawakosa nyota wake watatu kwenye mchezo wake wa kwanza wa Klabu Bingwa dhidi ya Rivers United kutoka nchini Nigeria unaotarajiwa kupigwa Septemba 12, 2021.

Wachezaji hao ni Khalid Aucho kutoka Uganda, beki kisiki Djuma Shaban na mshambuaji Fiston Mayele wote kutoka DR Congo.

Chanzo cha nyota hao kukosa mchezo huo ni baada ya kukosa hati ya uhamisho kutoka kwenye vilabu vyao vya awali.

Inasemekana Aucho amenyimwa hati hiyo na klabu yake ya huko Misri baada ya klabu hiyo kumtaka aongeze mkataba, lakini akagoma kufanya hivyo na kutimkia kunako wana wa Jangwani.

Kwa vilabu vya Union Maniema na AS Vita walipotoka Djuma na Fiston, havikutoa hati ya uhamisho kwa klabu ya Yanga kama inavyotakiwa na FIFA, moja ya sababu ikisemekana ni madeni inayodaiwa Yanga na vilabu hivyo.

“Klabu ya Yanga imefanya kila kitu kwa muda sahihi, kunasa sahihi ya Khalid Aucho ambaye alikuwa na mgogoro na klabu yake ya awali iliyoshindwa kumlipa mshahara wake hadi FIFA kuingilia na kuvunja mkataba wake na Aucho kuwa mchezaji huru,” Haji Manara

“Kwa Djuma halikadhalika tulifanya kila kitu kwa wakati, bahati mbaya walituma hati ya uhamisho siku moja baada ya dirisha la usajili kufungwa” aliendelea kusema Manara.

Manara ameendelea kusema kutokana na changamoto hizo, uongozi wa klabu ya Yanga wamewasiliana na TFF kuwaomba wawasiliane na FIFA kutafuta suluhu ya matatizo haya.

error: Content is protected !!