Yanga yasaini mkataba wa bil.12 na Sportpesa

HomeMichezo

Yanga yasaini mkataba wa bil.12 na Sportpesa

KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam, leo imesaini mkataba mpya wa udhamini na Kampuni ya Sportpesa, wenye thamani ya Sh Bil. 12.335 kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mkataba wa awali wa SportPesa na Yanga uliodumu kwa miaka mitano, ulimalizika hivi wiki chache zilizopita, lakini kampuni hiyo ya michezo ya kubahatisha ikaonesha nia ya kuendelea tena.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo iliyofanyika Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Utawala wa Sportpesa, Abas Tarimba amesema wamesaini mkataba huo baada ya kuridhishwa na mwenendo wa Yanga na pia kufuata masharti ya mkataba.

“Hii ni historia kwa klabu ya Yanga, kwani kwenye mkataba wa awali, thamani yake kwa miaka yote mitano ilikuwa Sh. Bil 5.2. Yanga itavuna zaidi ya Sh bilioni 4 kwa mwaka, ” amesema Tarimba.

Amesema pia Yanga watapata Sh Milioni 150 endapo watatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara, Sh milioni 112 kama watabeba ubingwa wa Kombe la FA na Sh Milioni 75 kama watatinga fainali ya FA.

Kwa upande wake Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, ameipongeza SportPesa kwa kufikia makubaliano hayo ambayo yameongeza thamani ya Yanga.

error: Content is protected !!