Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan leo Septemba 17,2023 amehitimisha Ziara ya Siku tatu Mkoani Mtwara ambapo Ziara hiyo imekuwa na Mafanikio Makubwa katika kutembelea na Kuzindua Miradi ya Maendeleo.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha Ziara hiyo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Bomani Masasi, Rais Samia ameshukuru Wananchi wa Mtwara kwa ukarimu na ushirikiano walioonyeaha kipindi chote Cha Ziara.
Aidha Rais Samia amewaahidi Wananchi wa Mtwara kuwa Serikali imedhamiria Kuleta Maendeleo kwenye Mkoa huo kwa Kuleta Miadi mingi ya Maendeleo.
Pamoja na hayo Rais Samia amewataka Viongozi anaowateuwa kumuwakilisha vizuri kwenye Maeneo yao kwa kusikiliza na kutatua kero na Changamoto za Wananchi.
Hata hivyo Rais Dkt Samia ametoa wito kwa Wazazi Mkoani humo kuacha kuwacheza watoto wa kike katika umri mdogo kwakuwa imekuwa chanzo Cha mimba za utotoni na badala yake amewataka kutimiza Mila hiyo kwa kuwacheza wakiwa kwenye umri wanaojitambua.
Baada ya kumaliza Ziara ya Kikazi Mkoani Mtwara, Rais Dkt, Samia atakuwa Mkoani Lindi ambapo atatembelea na Kuzindua Miradi mbalimbali ya Maendeleo.