Ziara ya Rais Samia Qatar yazidi kuvuta wawekezaji

HomeKitaifa

Ziara ya Rais Samia Qatar yazidi kuvuta wawekezaji

Tangu ashike kijiti cha kuiongoza Tanzania, Rais Samia Suluhu amekuwa akienda kwenye ziara mbalimbali nje ya nchi jambo lililo ibua mitazamo tofauti huku wengi wakitaka kuona matunda ya ziara hizo anazozifanya Mheshimiwa Rais.

Hatimaye, ziara yake aliyoifanya Oktoba, mwaka jana nchini Qatar, imeendelea kuvuta wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye sekta ya mifugo nchini.

Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Widam Food, Al Nouby Al Marri, wa Qatar kumtembelea Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega jijini Dodoma juzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Kiongozi wa Taifa la Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Kiongozi huyo Doha nchini humo tarehe 04 Oktoba, 2022.

Bw. Al Nouby alisema lengo la ziara yake ni kukamilisha hatua za kuanzisha kampuni ya Widam Food nchini ambayo inashughulika na biashara ya nyama.

“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutufungulia milango ya uwekezaji hapa Tanzania na sisi tunaona nyama ya Tanzania ina mustakabali mzuri kibiashara nchini Qatar,” alisema Al Nouby.

Waziri Ulega alisema serikali imedhamiria kuboresha uzalishaji wa sekta ya mifugo, hivyo ujio wa mkurugenzi  huyo unaunga mkono jitihada za serikali.

error: Content is protected !!