Ziara za Rais Samia nje ya nchi zaleta matunda

HomeKitaifa

Ziara za Rais Samia nje ya nchi zaleta matunda

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imechukua hatua kubwa kwa kutenga hekari 80 za ardhi huko Zanzibar kwa ajili ya nyota wa kimataifa wa filamu, Idris Elba, kujenga studio ya kimataifa. Hatua hii ina malengo makuu manne:

1. Kuongeza Uonekano wa Tanzania Kimataifa: Kwa kuwa na studio ya kimataifa ya filamu, Tanzania itapata fursa ya kuonekana na kutambulika zaidi kwenye jukwaa la kimataifa.

2. Kuitangaza na Kuiuza Tanzania: Studio hii itakuwa chachu ya kuitangaza Tanzania kama kituo cha ubunifu na utamaduni, hivyo kuongeza hadhi na sifa ya nchi yetu.

3. Kuboresha Soko la Filamu la Tanzania: Uwepo wa studio hii utaleta teknolojia na utaalamu wa hali ya juu katika sekta ya filamu, hivyo kusaidia kuboresha soko la filamu na kuongeza ubora wa filamu zinazozalishwa nchini.

4. Kuongeza Utalii Tanzania: Filamu na vipindi vya televisheni vitakavyotengenezwa katika studio hii vitavutia watalii kutoka pande zote za dunia kuja kutembelea Tanzania na kujionea uzuri wa nchi yetu.

Mama Samia anafungua milango ya kimataifa ili mamilioni ya Watanzania waingie kwenye uchumi wa dunia.

Wakati viongozi wa upinzani wakiwa kwenye safari za nje au wanapokuwa na wageni kutoka nje wanaiponda Tanzania na kushawishi serikali za kigeni kuzuia fursa kwa Watanzania, Mama Samia anafanya kinyume chake.

Hatua hizi zote ni sehemu ya juhudi kubwa za Rais Samia kutumia diplomasia kuleta fursa kwa Tanzania, fursa ambazo hapo awali zilikuwa zimefungika.

Rais Samia anaendelea kuonyesha kuwa Tanzania ni nchi yenye uwezo na nia ya kuwa sehemu muhimu katika jukwaa la kimataifa, ikifungua milango ya maendeleo na mafanikio kwa wananchi wake.

error: Content is protected !!