Zifahamu kazi ambazo haziathiriwi na teknolojia

HomeElimu

Zifahamu kazi ambazo haziathiriwi na teknolojia

Teknolojia inapokuja inakuwa na faida zake na hasara zake, ukuaji wa teknolojia haswa katika mataifa yalioendelea umepelekea kuwepo na roboti zenye uwezo wa kufanya kazi kama binadamu, pia kuwepo kwa mashine ambazo zinafanya kazi nyingi zilizokuwa zinafanywa na binadamu.

Hivyo inakadiriwa kuwa kwa miaka mitano mpaka 10 ijayo baadhi ya ajira zitapotea, zifuatazo ni ajira ambazo haziwezi kupotea sababu ya teknolojia:

Meneja mwajiri
Idara ya Rasilimali Watu ya kampuni siku zote itahitaji binadamu kusimamia mizozo kati ya watu ina muhitaji bianadamu kwa sababu binadamu wana ujuzi wa kutambua, kufikiri na kuzioelewa hisia za binadamu.

Wanasheria
Kuwa wakili kuna maanisha kuwa na akili ya kutosha kutafsiri sheria na kutoa utetezi kwa niaba ya mtu, hivyo inamuhitaji zaidi mwanadamu na akili ya kutosha.

Wabunifu wa Picha
Ubunifu wa picha unahitaji sanaa na ufundi, inahitaji uelewa kujua kile mteja wako anataka kwa sababu mahitaji ya kila mtumiaji ni ya kipekee.

Wakurugenzi watendaji
Watendaji wakuu wanapaswa kuangalia kwa umakini utendaji wa wafanyakazi wote katika ofisi pamoja na kuhamasisha timu kubwa za watu wanaowafanyia kazi.

Wanasayansi
Kuna mengi zaidi kwa mwanasayansi kuliko kufanya tu majaribio na tafiti. Uvumbuzi hauwezwi kufanywa na roboti wala mashine hivyo ina muhitaji mwanadamu. Sambamba na taaluma hizo zingine ni waandaa matukio, waandishi, afisa mahusiano na watengenezaji wa programU.

error: Content is protected !!