Zijue rangi 7 za mikojo na maana zake

HomeElimu

Zijue rangi 7 za mikojo na maana zake

Haja ndogo/mkojo hutoka kwa rangi tofauti, na rangi hizi ni ishara juu ya maendeleo ya afya zetu. Mabadiliko ya rangi ya mkojo yanaweza kusababishwa na aina vyakula tunavyokula hata aina za dawa tunazotumia kunywa. Hatupaswi kupuuza rangi za mikojo yetu kwani ni ishara tosha  zinazotuandaa kuyakabilia maradhi mbalimbali yanayotenyemelea.

Tafsiri nyuma ya rangi ya mikojo

  1. Rangi Nyeupe
    Mkojo huu ni ishara kuwa unakunywa maji mengi, hii nzuri kwa afya yako na inapunguza uwezekano wa kupata maradhi ya figo na njia ya mkojo.
  1. Mkojo wenye povu jepesi
    Kuna muda unaweza kukojoa povu jepes na mkojo mzito kiasi. Rangi yake inaweza kuwa manjano iliyopauka sana, hii ni dalili kubwa ya UTI. Dalili ya rangi ya mkojo huu inaweza kuwa ni ongezeko la madini fulani mwilini au dalili ya ugonjwa wa figo. Kukojoa mkojo wa povu pia huweza kuwa dalili ya kupungukiwa maji mwilini. Watu wanaopenda kula nyama nyekundu kwa wingi hutokwa na mkojo wa aina hii.
  2. Manjano iliyofifia/dhahabu
    Moja ya dalili ya kuwa afya yako iko vizuri ni kukojoa mkojo wa manjano iliyofifia au dhahabu.
  1. Njano inayong’aa (angalia Amber Urine)
    Mkojo wa manjano inayonga’aa (amber urine) ni mkojo unaoonesha ishara kuwa mtu hutumia sana vyakula vyenye vitamini zaidi ya kiwango kinachohitajika mwilini. Hii sio mbaya kwa afya, lakini ni vyema kumuona tabibu kujua ni aina gani za vitamini unapaswa kutumia kwa wingi na zipi za kupunguza
  1. Mkojo wa Ugoro
    Mkojo wa rangi ya ugoro ni dalili kuwa mwili umepungukiwa maji kwa kiwango kikubwa sana au mtu ameanza dalili za ugonjwa wa ini. Kwa wenye saratani aina ya ‘melanoma’, saratani inayoathiri sehemu ya seli ambazo hutengeneza ngozi ya mwili. Saratani hii husababisha rangi inayotengenezwa kuyeyuka na kuingia kwenye mfumo wa maji mwilini hivyo kusababisha kukojoa mkojo unafanana na ngozi ya mwili wa mtu.
  1. Mkojo wa pink/mwekundu
    Mkojo huu ni hatari, inaonesha kuwa mkojo wako una damu na moja ya ishara kubwa zaidi ya ugonjwa wa figo, UTI au jereha kwenye tezi dume.  Lakini kukojoa mkojo mwekundu kuna muda inaweza kuwa ulaji wa zabibu kwa wingi au mkojo huu pia hutoka kutokana na mtu kufanya kazi inayotumian nguvu nyingi sana.
  1. Mkojo wa kijani
    Mkojo wa aina hii ni nadra watu kukojoa, unaweza kubabishwa na hali fulani ya vinasaba au moja ya dalili za ugonjwa wa UTI. Mkojo wa kijana unaweza kusababishwa pia na aina ya vyakula yenye rangi ya kijani au aina ya dawa ambazo mtu hunywa kwa minajili ya kupunguza maumivu.
error: Content is protected !!