Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amempa pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kuwaunganisha Watanzania pamoja na vyama vya siasa.
Zitto ametoa pongezi hizo kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma wakati Rais Samia Sulu akizungumza na wananchi wa mkoa huo leo tarehe 18 Oktoba,2022.
“Napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza sana kwa juhudi kubwa zinazofanyika kuwaweka Watanzania pamoja bila kujali itikadi zao kuwepo kwangu hapa ni ishara hiyo,” amesema Zitto.
Pia, amempongeza Rais Samia kwa kutumia njia bora ya uongozi ya kuunganisha vyama vya siasa kwa kukutana nao na kujadili masuala ya kujenga taifa uamuzi alisema umepelekea kuwepo kwa utuli wa hali ya siasa nchini.
“Hakuna njia yoyote yakuifanya nchi yetu iweze kwenda mbele isipokuwa njia hii ambayo unaipita yakujenga maridhiano ya kitaifa na kwa hili kwa niaba ya viongozi wenzangu wote wa kisiasa nchini tunapenda kukupongeza na kukushukuru sana,” amesema Zitto.
Ikumbukwe, tangu aingie madarakani mwezi Machi mwaka 2021, Dhamira kuu ya Rais Samia Suluhu ni kujenga nchi kupitia maridhiano jambo ambalo tunaona akilifanya kikamilifu kwa kukutana na viongozi wa vyama pinzani na kujadiliano nao.