4R isiwe kisingizio kuvunja sheria

HomeUncategorized

4R isiwe kisingizio kuvunja sheria

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kutotumia falsafa ya 4R (Maridhiano, Mageuzi, Ustahimilivu na Kujenga Upya) kama kisingizio cha kuvunja sheria au kujenga mazingira yanayohatarisha amani, usalama na utulivu wa nchi.

Amesisitiza kwamba utekelezaji wa falsafa hiyo unaenda sambamba na uzingatiaji wa katiba na sheria za nchi.

Rais alieleza hayo jana usiku akihutubia Taifa katika shamrashamra za miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

“Kutekelezwa kwa falsafa ya R4 kunaendana sambamba na kuzingatiwa kwa katiba na sheria za nchi. Kamwe, falsafa hii haiwezi kuwa kisingizio cha kuvunja sheria au kujenga mazingira yanayohatarisha amani, usalama na utulivu wa nchi yetu,” alisema.

Aidha, Rais Samia alisema kuputia falsafa ya 4R, demokrasia ya Tanznaia imeimarika na alisisitiza kuwa falsafa hiyo itumike kuwa nyenzo muhimu katika kukuza ushiriki na ushirikishaji wa wananchi

error: Content is protected !!