Mchezaji wa Serengeti Girls gumzo mtandaoni

HomeBurudani

Mchezaji wa Serengeti Girls gumzo mtandaoni

Mchezaji wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 – Serengeti Girls, aliyeifungia Tanzania magoli matatu kati ya manne kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia iliyochezwa dhidi ya Cameroon ameendelea kuwa gumzo mara baada ya mechi hiyo kukamlika bada ya watu haswa wa Cameroon kulinganisha uchezaji wake na muonekano wake.

Clara Cletus Luvanga (16) ambaye pia anaichezea timu ya Yanga Princesses, ana uwezo mkubwa wa kucheza mpira wa miguu, huku watu wakilinganisha uwezo wake huo mkubwa na ule wa wachezaji wa kiume.

Binti huyo  alilazimishwa kwenda kuangaliwa jinsia yake na daktari baada ya wachezaji wa Cameroon kusema kuwa “hafanani na msichana”.

Tovuti ya Cameron Tribune imeandika habari hiyo na kusema “Kabla ya kuanza kwa kipindi cha pili, mwonekano wa Clara Cletus Luvanga ulizua wasiwasi lakini hilo uhalisia wa mchezo. Kimwili, Watanzania walikuwa na nguvu zaidi hasa kwenye mashambulizi na hilo lilichangia kuwatawala Wacameroon.”

Hadi sasa Luvanga ndiye mfungaji bora zaidi wa kike kwenye mechi za kufuza Kombe la Dunia kwa kufunga jumla ya magoli 10.

Je! Cameroon wangeshinda wangekuwa na sababu zote hizo? Kabla ya mchezo kuanza hawakuona haja ya kuangalia jinsia ya mchezaji? Ikumbukwe kuwa kila mtu huja na upekee na kipaji chake.

error: Content is protected !!