Mwili wa Mkaguzi Mkuu wa Huduma ya Wanyamapori ya Kenya (KWS) wakutwa kati ya vifurushi vilivyookolewa Mto Yala.
Wananchi wa Kenya wazidi kuililia serikali kutatua changamoto ya miili ya watu inayookotwa Ziwa Yala kwa takribani mwaka mmoja sasa huku wengine wakiendelea kuripoti kupotelewa na ndugu zao.
Machi 18, mwili wa Ofisa wa KWS, Francis Oyaro aliyepotea miezi sita iliyopita uliokotwa ukielea katika mto huo ikiwa ni miongoni mwa miili takribani 40 iliyookotwaikielea katika mto huo kwa kipindi cha chini ya miezi sita.
Miili hiyo hutupwa katika mto huo imeonekana kuwa “Imepakiwa vizuri na kufungwa kama kifurushi,” Okero Kite mwananchi aishiye karibu na mto huo na kuokoa zaidi ya miili 31 kwa kipindi cha miezi sita alieleza.
Huzuni inazidi kutanda kwa familia ya Onyaro kwani mwaka 2010 binamu wa Francis aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Utumishi Mkuu (GSU), Konstebo Jorim Odhiambo Abang alitoweka katika mazingira ya kutatanisha na hajawahi kuonekana tena.
Katika miili iliyotupwa Mto Yala mingi inaonekana kuwa na majeraha yanayoonesha kuteswa sana kabla ya kufariki ikiwemo kukatwa, kufungwa kwa kamba na wengine wakiwa wamevalishwa mifuko ya plastiki kichwani.
Watekelezaji wa mauaji hayo bado hawajajulikana, huku ikisemwa kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi. Huku shuhuda wakisema huweza kusikia mngurumo wa gari wanaloamini hutupa miili hiyo usiku wa manane ama mapema alfajiri.
Polisi wazidi kuwasihi wale waliopoteza ndugu zao kujitokeza kuweza kutambua miili iliyohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja mjini hapo.