TMDA: Marufuku sigara hadharani

HomeKitaifa

TMDA: Marufuku sigara hadharani

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Kanda ya Kati, Sonia Mkumbwa ameeleza kuwa watumiaji wa bidhaa za Tumbaku watatakiwa kutengewa maeneo maalum ili kulinda Afya za watu wengine wasiotumia.

Amesema ni marufuku matumizi ya sigara na bidhaa za Tumbaku katika maeneo yasiyo rasmi na maeneo ya hadhara.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku  kifungu cha 12(2), maeneo yasiyoruhusiwa ni pamoja na maktaba, sehemu za ibada, kambi, katika shughuli za michezo na burudani na sehemu zinazouza vyakula, ofisi, vyombo vya usafiri, mabanda ya maonesho, masoko, maduka na sehemu nyingine maalum kwa ajili ya kukutania watu.

Pia alisema, kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu yeyote anayemiliki maeneo yaliyokatazwa anapaswa kutenga sehemu kwa ajili ya wavutaji.

“Chumba kitakachokuwa kimetengwa kwa ajili ya uvutaji Sigaŕa kitatakiwa kuwa na mfumo wa kutolea moshi nje na kuweka maandishi ya ‘No Smoking’ na ‘Haiŕuhusiwi kuvuta Sigaŕa’ katika maeneo pasipoŕuhusiwa,” inasema sheŕia hiyo.

error: Content is protected !!