Uchunguzi na matibabu ya TB ni bure

HomeKitaifa

Uchunguzi na matibabu ya TB ni bure

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema serikali imefuta gharama za uchunguzi kwa wagonjwa wote wenye dalili za kifua kikuu waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi na kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kifua kikuu duniani ambapo kimataifa yamefanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga, Waziri Ummy alisema takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2021, kulikuwa na wagonjwa 47,000 ambao hawakuweza kufikiwa na huduma na hivyo bado wapo kwenye jamii wanaendelea kuambukiza watu wengine.

“Hivyo ili tuweze kuwapata wagonjwa wote hao, kuanzia sasa naelekeza nchi nzima uchunguzi wa kifua kikuu ni bure. Ni marufuku mgonjwa ambaye anafika kwenye vituo vya afya na hospitali kulipishwa,” alisema Ummy.

Aidha , Waziri Ummy alisema ili kuhakikisha wagonjwa wanaotoka kwenye kaya duni wanaendelea na matibabu bila ya uchumi wao kutetereka, serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanakuja na mpango wa kuwezesha kaya maskini zenye wagonjwa sugu wa TB.

error: Content is protected !!