Umaarufu wake kwenye siasa ulimfanya Abdulrahman Kinana azidi kuwa maarufu kwenye jamii na zaidi kati ya wanachama wa CCM.
Leo hii Machi 31, 2022 katika ukumbi wa White House, Dodoma Kinana ameteuliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara baada ya Philip Mangula, aliyekuwa akishikilia nafsi hiyo kujiuzulu akiwa na miaka 81.
Kwa miaka 20 hadi kufika 1992, Kinana alikuwa akilitumikia Jeshi la Tanzania na kustaafu katika cheo cha kanali.
Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa lakini pia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kinana ndiye Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki kuanzia mwaka 20221 hadi 2006. Mwaka 2012 Kinana alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa hadi alipojiuzulu 2018. Kwa miaka 10 pia aliliwakilisha Jimbo la Arusha bungeni.
Akizaliwa kwenye asili ya kisomali, Kinana alijipatia shahada ya kwanzaSayansi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Ljubljana, Yugoslavia na baadaye kusomea Shahada ya Uzamili kuhusiana na utawala wa umma (MPA) kutoka Chuo Kikuu cha Havard, Marekani.