Neema imeanza kufunguka kwa wafanyabiashara wadogo(MACHINGA) baada ya kusaini mkataba wa shilingi bilioni 200 zilizotengwa na benki ya NMB kwa ajili ya kuwakopesha ndani ya miaka mitano, hatua iliyokuja baada ya hivi karibuni Rais Samia Suluhu kuziagiza taasisi za fedha kuwa na programu maalumu zitakazo wasaidia wamachinga kukopa kwa gharama nafuu.
Mwenyekiti wa Umoja wa Shirikisho la Wamachinga Tanzania , Ernest Masanja alimshukuru Rais Samia Suluhu na kuwataka wafanyabiashara hao kukaa kwenye vizimba vyao ili fursa kama hizi zisiwapiti.
“Nina washauri wamachinga wote wasiache kukaa katika vizimba walivyopangiwa watakosa fursa nyingi, Rais Samia aliona wamachinga wakikaa barabarani hawatoweza kukopeshwa,
“Kwa sasa Rais Samia anajipanga kuja kutengeneza maeneo ya Wamachinga, kwahiyo kila mfanyabiashara akakae katika eneo lake na asiliache, nawasihi wafanye hivyo ili waweze kukopesheka, wasije kulalamika kuwa sina mtaji fedha zipo nje nje ,”alisema Masanja.