Wananchi kwa kushirikiana na wataalam wa maji wanaendelea na zoezi la kutafuta miili ya watu waliozama katika Mto Mori uliokuwa ukifurika jumamosi, majira ya saa nne asubuhi.
Watu kumi waliokuwa wamepanda mtumbwi wakitokea kijiji cha Mori kuelekea Matara walizama huku watano wakiokolewa siku hiyo hiyo na wengine wasipatikane.
Hadi kufikia jana wananchi walifanikiwa kuopoa miili mingine miwili mmoja ukiwa ni wa mtoto na zoezi la kuendelea kutafuta miili iliyosalia linaendela.
“Walikuwa wakivuka mto kutoka kijiji cha Mori kwenda kijiji cha Matara,” alisema Godfrey Dalmas, Diwani wa kata ya Nyathorogo, Rorya.
Kikosi cha wazamiaji kilifika eneo hilo na kushirikiana na wananchi wakiendelea kusaka miili mingine.
Kufuatia zoezi hilo, wananchi wanaiomba serikali kujenga daraja juu ya mto huo ili kuepusha ajali za namna hiyo.