Waziri: Aliyenajisi mtoto na kukimbia naye atafutwe

HomeKitaifa

Waziri: Aliyenajisi mtoto na kukimbia naye atafutwe

Baada ya kufika jijini Arusha kwenye ziara fupi ya uhamasishaji wa Siku ya Kimataifa ya Familia, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima ameagiza Jeshi la Polisi la mkoa huo kumsaka Ally Abdallah anayedaiwa kutoweka na mtoto wake wa kike wa miaka minne baada ya kumnajisi na kuharibu vibaya sehemu za siri.

“Kweli nilishtuka nikaamua kumfuata mama huyu eneo la Uswahilini jijini Arusha na nimeongea naye analia sana lakini nimemwaambia wataalamu wa kisaikolojia wasaidie kwanza arudi kwenye hali yake,” alisema Waziri Gwajima.

Waziri Gwajima alisema inasikitisha kuona wakati nchi inajiandaa na maadhimisho ya siku hiyo, yenye kuhamasisha amani na upendo kwenye familia, kuna baadhi ya watu wamekutana na ukatilii wa kijinsia na kuamua kumuachia Mungu badala ya kupeleka kwenye vyombo husika.

Mama mzazi wa huyo, Amina Abdallah (25) amesimulia tukio hilo na kusema mtoto wake alinajisiwa siku ya ya sikukuu ya Idd El Fitri.

“Baada ya kumuona mtoto wangu katika hali hiyo nilimuuliza kafanya nini akanijibu ameumizwa na kijiti. Nikamtishia nikamwambia usiponiambia ukweli nitajichoma kisu nife bado mtoto akazidi kusema amechomwa na kijiti,” alisema.

Mama huyo hakulizika na majibu hayo hivyo aliamua kumpeleka mtoto kwa majirani ili wamsaidie kuumuliza mtoto amepatwa na nini lakini hakusema chochote na ndipo aliamua kumchapa kidogo akakojoa majimaji mazito meupe.

“Kutokana na maji hayo tulimkagua na ndipo tukabaini amebakwa na kuharibiwa vibaya hali iliyotulazimu mimi na mama yangu mzazi na majirani kwenda kituo kidogo cha polisi Uga Ltd na kupewa fomu namba tatu kisha tukaenda Hospitali ya Rufani ya Mount Meru kwa ajili ya matibabu,” alisimulia Amina.

Aidha, kuhusu kilio cha mama mzazi wa mtoto huyo cha kuomba kusaidiwa kurudushiwa mtoto, kuwezeshwa kiuchumi na mahali pa kuishi, Dk. Gwajima aliagiza halmashauri impatie mkopo kupitia mikopo ili ajikwamue kiuchumi.

error: Content is protected !!