Wizara ya Afya Tanzania imesema hayupo wala hajawahi kuwepo Mgonjwa wa homa ya nyani Nchini Tanzania (Monkeypox) lakini hata hivyo imetaka Watu wote kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na kuzuia magonjwa ya kuambukizwa na yale ya mlipuko ikiwa ni pamoja na usafi binafsi na wa mazingira.
Katika taarifa yake, Wizara ya Afya imewataka pia Wananchi kutogusa au kula mnyama anaeumwa au mzoga na vilevile kutogusa vitu vilivyotumika na mnyama mgonjwa au mzoga.