Morocco na Sudan zinachunguza visa vinavyoshukiwa vya ugonjwa wa monkeypox, imesema taasisi hiyo ya afya barani.
Hii inakuja baada ya milipuko ya virusi kubainika hivi karibuni barani Ulaya, Australia na Mashariki ya Kati.
Monkeypox kwa kawaida huhusiana na safari za kuelekea katika maeneo ya kati na magharibi mwa Afrika, karibu na misitu ya kitropiki, lakini baadhi ya visa vipya havina uhusiano wowote na safari.
Wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari Dkt Ahmed Ogwell, naibu mkurugenzi wa Taasisi ya udhibiti wa magonjwa (CDC) alithibitisha kuwa hapakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na safari za kuelekea maeneo yanayohusishwa na Monkeypox.
Alisema kuwa bara la Afrika hadi sasa limeripoti visa1,405 na vifo 62 vinavyohusiana na monkeypox- mwaka huu-kikiwa ni kiwango cha 4.4%.
Watu hawa wenye Monkeypox walipatikana katika nchi nne ambako maradhi haya nadra yalipatikana : Cameroon, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Nigeria.
Dkt Ogwell amesema kuwa nchi zote za Kiafrika zimeshauriwa kuongeza kiwango chake cha ufuatiliaji na upimani wa ugonjwawa Monkeypox.
Monkeypox, ambayo ni maambukizi ambayo sio makali sana, yanaweza kusambaa wakati mtu anakaribianana mtu mwenye maambukizi.
Dalili za mwanzo ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, uvimbe, maumivu ya mgongo. Maumivu ya misuli- na upele unaweza kujitokeza wakati homa inapojitokeza.
Inadhaniwa kuwa inasambaa kwa panya, na kindi.
Kunawa mikono ni muhimu sana kwani ni ugonjwa unaosambaa kwa kusalimiana ” Dkt Ogwell alisema.
Pia ameshauri watu kuepuka kuwagusa Wanyama wanaoonekana kuumwa na wale wanaofahamika kubeba virusi vya maambukizi.
Chanjo ya tetekuwanga inatolewa Afrika, Dkt Ogwell amesema.
“Chanjo iliyopo ya tetekuwanga itapewa kipaumbele kwa wahudumua wa afya na maeneo yaliyothibitishwa kuwa na virusi hivyo,” alisema.