Kuna imani potofu za kiafya kwenye jamii ambazo zinaendelea kuaminika kuwa ni ukweli licha ya tafiti kufanyika na kubaini kuwa hazina ukweli wowote.
Baridi husababisha mafua
Wengi huamini kuwa kunywa maji ya baridi, ama kupigwa na baridi huleta mafua. Uhalisia ni tofauti kwani virusi vinavyosababisha mafua husambaa kwa urahisi kwenye hali ya ubaridi na vilevile watu hupenda kukaa zaidi ndani na kufanya virusi hivyo kuenea kusambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Baridi huchochea na si kusababisha.
UKIMWI ulisababishwa na mtu kujamiiana na nyani
Ni moja ya theory kadhaa juu ya kuenea kwa ugonjwa wa UKIMWI japo zinazoaminika zaidi ni kwamba wawindani waliathirika baada ya kula nyama ya nyani na kwamba pengine waligusa damu ya nyani mwenye virusi wakiwa na vidondo.
Kula ‘Chocolate’ huongeza hamu ya tendo
Hakuna utafiti wowote unaoonesha kuwa wanawake wanaokula chocolate wanakuwa na hamu ya tendo zaidi ya wale wasiokula chocolate. zaidi sana pengine inakusaidia kuhisi hivyo kutokana na kuweka mawazo yako kufikiri hivyo.
Sukari husababisha mtoto kuchangamka
Wengi huamini kuwa mtoto anapokunywa vitu vya sukari huchangamka zaidi japo tafiti nyingi zinapinga hilo na hiyo haimaanishi kuwa sukari ni nzuri kwa afya ya mtoto. Zipo pia tafiti zinazoonesha sukari husababisha kuongezeka uzito kwa mtoto anayekula vyakula vya sukari sana. Miaka ya 1970 yupo mwanasayansi ambaye aliondoa sukari kwenye lishe ya mtoto na kusema kuwa tabia ya yule mtoto ilizidi kuwa nzuri.
Gegedu huwapata wazee tu
Theluthi mbili 2/3 ya wanaoathiriwa na gegedu (arthritis) ni wenye umri chini ya miaka 65. Kuna zaidi ya 100 aina za ugonjwa unaoshambulia gegedu ambayo huathiri watu wa rika zote. Huathiri karibu watoto watatu katika kila watoto 1,000.