Shehena nyingine ya chanjo aina ya Sinopharm dozi milioni tatu zimeingia nchini ambazo zitawakinga Watanzania 1,500,000 dihi ya ugonjwa wa Uviko-19.
Chanjo hizo zimetolewa kwa hisani ya mke wa Rais wa China, Prof. Peng Liyuan.
Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya, Dk. Beatrice Mutayoba, alisema mpaka sasa zimetolewa kutoka China zimefikia dozi 6,000,000.
Alisema chanjo hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na kuwataka wananchi wachanje kwa sababu ili kufikia kinga jamii ni lazimi asilimia 70 ya walengwa ambao ni watu 21,518,649 wawe wamechanja.
Dk. Mutayoba alisema hadi kufikia Julai 12, mwaka huu, Watanzania 10,511,804 sawa na asilimia 32.91 walikuwa wamekamilisha dozi ya Uviko-19 na zilizopokelewa ni 21,226,520.
Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania, Chu Kun, alisema mke wa Rais wa China Prof. Peng, amependekeza kutoa chanjo kwa wanawake, watoto na vijana katika nchi 53 za Afrika na sehemu ya chnajo hiyo itatolewa kwa kundi hilo nchini Tanzania.