Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema serikali itatoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara iliyotoka katika mishahara ya mwezi Julai, 2022 nakuwataka wananchi kuwa na subra.
“Ndugu wafanyakazi naomba tutulie, Serikali itatoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara iliyotokea katika mishahara ya mwezi Julai, 2022,” Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameandika katika akaunti yake rasmi ya twitter.
— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) July 22, 2022
Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilitangaza kuongeza kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3 kuanzia Julai 1. Kwa maana hiyo, watumishi walikuwa wanategemea kuona mabadiliko katika mishahara yao.