Tanesco yasitisha mfumo wa Nikonekt

HomeKitaifa

Tanesco yasitisha mfumo wa Nikonekt

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema linafanya maboresho ya mfumo wa Nikonekt kwa siku mbili leo na kesho.

Taarifa ya ofisi ya uhusiano Tanesco, makao makuu ilisema Shirika hilo linawatangazia wateja wake wote kuwa kutakuwa na maboresho ya mfumo wa Nikonekt kwa siku mbili kuanzia Julai 23 hadi 24, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maboresho hayo ni muhimu na yanalenga kuongeza ufanisi kwenye mfumo na kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wake.

Ilisema katika kipindi hicho maombi ya umeme hayatafanyika isipokuwa kwa maombi ya dharura yatakayopokelewa kupitia kituo cha miito kwa namba 0748880000

“Shirika linawashukuru wateja wetu kwa muitikio mkubwa wa matumizi ya mfumo wa Nikonekt na tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kipindi hiki cha maboresho ,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

error: Content is protected !!