Majaliwa : Serikali ipo pamoja na nyie

HomeKitaifa

Majaliwa : Serikali ipo pamoja na nyie

Serikali imesema nyongeza ya mishahara 23% iliyotangazwa mwaka huu 2022, inawalenga watumishi kati asilimia 75 hadi 78 wanaopokea mishahara midogo, na siyo wenye mishahara mikubwa kama vile Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa.

Ufafanuzi huo umetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo tarehe 29 Julai 2022 na kusema kwamba ni kweli kwamba 23% iliyotamkwa haijalipa watu wote na ni kwasababu wa kanuni inayotumika katika kutamka viwango vya mishahara na kinapotamkwa wanaonufaika si wote mpaka wa mishahara mikubwa, wanaonufaika ni wale wa kada ya chini.

“Hao wanaosema kwamba tumeongeza sh 20 ni wenye mishahara mikubwa, wako kwenye hii asilimia 22, huku ndiyo utawakuta Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mameneja, Wakurugenzi na Wakuu wa mikoa ambao kidogo wana mshahara unaotosha,”-  amesema Waziri Mkuu

“Nataka niwaambie hata kama asilimia hii haikidhi. bado dhamira ya serikali ya kuboresha maslahi ya watumishi ambayo Rais ameionesha na hatua alizozipitia tuna matumaini huko baadaye tunaweza kufikia hatua nzuri,”- amesema Waziri Mkuu.

“Tunaposema tunapandisha mishahara kima cha chini, maana yake wanaangaliwa sana wale wafanyakazi wa kipato cha chini, ile asilimia inayotamkwa inawalenga zaidi wale wa kima cha chini,”amesema  Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu amewahakikishia kwamba serikali ipo pamoja nao na kuwasisitizia kuzidi kuiamini serikali kwani kila kinachofanywa ni kwa manufaa yao.

 

error: Content is protected !!