Baadhi ya viongozi wa dini wakiwamo maaskofu, wameibuka na kutoa kauli kuhusu kitendo cha klabu ya Simba kuruhusu wato burudani kuingia na jeneza lilikoluwa limembeba msanii Tunda Man.
Kutokana na kitendo hicho, viongozi wa dini na wadau mbalimbali wameibuka na kushutumu kitendo hicho huku baadhi wakisema ni dhihaka ya dini ya Kikirsto ba kinapaswa kulaaniwa.
Askofu Msaizidi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Dk. Methodius Kilaini, alisema kitendo hicho ni kibaya na kinapaswa kukemewa.
“Hiki ni kitendo kibaya ambaco kinadhalilisha dini na imani za watu. Hakipaswi kuendelea kuwapo kwa mara nyingine hata kama ni masuala ya michezo,” alisema Askofu Kilaini.
Naye Askofu wa Tanzania Assembles of God (TAG),jimbo la Kigoma, Mulenda Kalama, alisema kitendo hicho ni kibaya na kwamba kinaashiria jambo baya kutokea.
“Hiki ni kitendo kibaya ambacho kinapaswa kukemewa na kila mtu. Hata kama ni masuala ya mpira, huwezi kubeba jeneza na ukaweka msalaba juu,” alisema Kalama.
Naye mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Mashariki ba Pwani(DMP) ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kitendo hicho hakikubaliki na kusisitiza kuwa “huyu dodo (Tunda Man) kajitabiria mwisho wake, ni suala la muda tu”.