Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameshangazwa na baadhi ya hospitali kuwatoza wagonjwa kiasi cha shilingi 15,000 ili kuweza kumuona daktari jambo ambalo si sawa na kuahidi kuchukua hatua ili kupunguza garama zisizo za lazima kwa wananchi.
“Nimeona tatizo moja kumuona daktari ni Shilingi elfu kumi na tano HAPANA,Elfu kumi na tano hii ni ya nini? Kwasababu daktari tunakulipa mshahara, kwa hiyo hili nalifanyia kazi nchi nzima”-Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy amesema hayo jana wakati wa ukaguzi wa Majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ambayo Rais Samia Suluhu Hassan Jana amekagua Ujenzi wa miundombinu iliyojengwa Hospitalini hapo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 27.