Watu wengi wanatumia kondomu kama kinga ya kujilinda dhidi ya magonjwa ya zinaa na wengine kuepuka kupata mimba lakini ukweli ni kwamba kondomu zina madhara yake endapo hazitotumiwa kwa ufanisi.
Zifuatazo ni madhara unayoweza kupata utumiapo kondomu wakati wa tendo la ndoa.
1. Mzimo (Allergy)
Maji maji yanayopatikana ndani ya kondomu yanatokana na nguni ya kwenye miti hivyo muda mwingine yanaweza yasiwe rafiki kwa mtumiaji na kumsababishia muwasho, vipele, kuumwa na kichwa au hata kizunguzungu.
Hivyo basi unapaswa kuwa makini pindi utumiapo kondomu.
2. Uwezekano wa kupata mimba zisizo tajariwa
Kumbuka, kondomu pia zinaweza kusababisha ukapata mimba bila kutarajia na hii ni kutokana na umakini wakati unapokuwa ukishiriki tendo la ndoa. Kondomu inaweza kutoka au kupasuka bila kujua.
Kuepuka hili unapaswa kuwa makini lakini pia ununuapo kondomu angalia muda wake wa kuharibika kwani endapo zitakuwa zimekwisha muda huwa zinakuwa nyepesi hivyo rahisi kupasuka.
3. Kupata magonjwa
Kondomu ni maalum kwa ajili ya kujilinda dhidi ya UKIMWI na magonjwa mengine lakini haiwezi kukulinda dhidi ya magonjwa mengine ya zinaa hasa yanayopatikana nje ya ngozi.
Hivyo basi unapaswa kuwa makini wakati wa kushiriki tendo la ndoa hata kama mtatumia kondomu kwani haiwezi kufunika sehemu yote ya ngozi.