Tanzania kumpa ushirikiano Ruto

HomeKimataifa

Tanzania kumpa ushirikiano Ruto

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema ataendelea kufanya kazi na Rais mteule wa Kenya, Dk. William Ruto, kudumisha uhusiano wa kihistoria na undugu baina ya Tanzania na Kenya.

Pia, Rais Samia amempongeza Dk. Ruto kwa kuthibitishwa na Mahakama ya Juu nchini humo kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa Rais uliofanyika Agosti 9, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa katika mtandao wa kijamii wa Twitter kupitia kwenye akaunti ya Rais Samia Suluhu ilieleza;

Juzi mahakama hiyo nchini Kenya, ilibariki ushindi wa Ruto, baada ya kutoa uamuzi wa maombi ya kikatiba yaliyofunguliwa na mgombea urais aliyeshindwa, Raila Odinga aliyekuwa akipinga matokeo.

Majaji saba wa mahakama hiyo kwa kauli moja walizikataa hoja zote tisa za kupinga ushindi wa Ruto, hivyo anakuwa Rais wa tano wa nchi hiyo.

Kufuata uamuzi huo, watuma maombi Raila Odinga na Martha Karua, walisema wanaheshimu utawala wa sheria na kuiheshimu mahakama.

 

error: Content is protected !!