Faida za bima ya afya kwa wote

HomeKitaifa

Faida za bima ya afya kwa wote

Serikali imewaomba wananchi kuunga mkono suala la bima ya afya kwa wote na kupuuza vitisho juu ya suala hilo kwa kuwa ni mkombozi kwa Watanzania.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi alisema hayo wakati akifungua kikao cha wakurugenzi wa wizara na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

“Wananchi wasitishwe na wala wasiogope juu ya sheria hii, tunahitaji kila Mtanzania awe na bima ya afya na hata kwa wananchi wasio na uwezo, serikali imeweka mazingira ya kuwatambua na kuwapa kadi maalumu za kupata huduma za matibabu hivyo tuunge mkono suala hili ambalo ndio mkombozi mkubwa katika afya zetu,”alisema Makubi.

Prof. Makubi alisema madhuni ya kutungwa kwa sheria hiyo ni kutokana na kuwapo kwa upungufu wa kiesheria katika Mfumo wa Bima ya Afya uliosababisha idadi kubwa ya wananchi kutokuwa na bima ya afya hivyo kukosa uhakika wa kupata huduma za matibabu.

Alisema sheria itawezesha wananchi wengi kuwa katika mfumo hivyo kuwa na uhakika wa kupata matibabu.

 

error: Content is protected !!