Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amekutana na timu ya dharura ya kukabili maambukizi ya magonjwa ya mlipuko katika Mkoa wa Dar es Salaam ili kuona utayrai wao kukabili tishio la ugonjwa wa Ebola.
Ummy alikutana na timu hiyo jana katika kituo maalumu cha kuhudumia wagonjwa wa magonjwa ya mlipuko katika Hopsitali ya Mkoa wa Temeke.
“Lengo langu kubwa kuja hapa ni kuangalia utayari wetu, tukipata mgonjwa leo hapa Dar es Salaam tunampelekea wapi? Nimpongeze Mganga Mkuu wa Dar es Salaam na timu yake tayari wameshajiandaa kwa kituo hiki hapa cha Temeke ambacho ndicho tulikitumia wakati wa COVID-19,” alisema.
Waziri Ummy alisema alipokea taarifa kutoa kwa Waziri wa Afya wa Uganda kuwa mpaka kufikia mwishoni mwa wili iliyopita, wagonjwa wapya watano wa Ebola walithibitishwa na kufanya jumla ya wagonjwa 126 huku 54 wakiwa waliolazwa na vifo vikifikia 12.
Alisema mwamnzoi wasiwasi wa tishio la maambukizi lilikuwa kwa MKoa wa Kagera lakini kupatikana kwa wagonjwa wapya katika jiji la Kampala kumeibua wasiwasi wa tishio la maambukizi kwa mkoa wa Dar es Salaam.
“Wasiwasi umeongezeka kwa sababu sasa ugonjwa umeingia Kampala, ndege zinasafiri, mabasi yanakuja Dar kutoka Kampala. Tuna takribani mabasi kumi yanayotoka Kampala kila siku,” alisema Ummy.
Sambamba na kutengwa kwa vituo hivyo, Waziri Ummy alimse serikali inakusudia kufanya kikao na waganga wajadi ili kuwapa uelewa ili kudhibiti tabia ya baadhi ya wagonjwa kutoroka hospitali na kukimbilia kwa waganga hao.