Serikali imesema makali ya mgao wa umeme nchini yanaweza kupungua mwezi ujao wa Novemba baada ya kukamilika kwa miradi ya umeme ukiwemo wa Kinyerezi I uliopo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameliambia Bunge jana Novemba 2, 2022 jijini Dodoma kuwa mwezi ujao mradi wa Kinyelezi I utakamilika na kuingiza megawati 185 katika gridi ya Taifa.
Amesema megawati hizo zitapunguza makali ya mgawo wa umeme unaendelea hivi sasa katika maeneo mbalimbali nchini ambao umeibua mjadala mpana miongoni mwa Watanzania wakiwemo Wabunge.
Aidha, Serikali ina mpango wa kutenga Sh500 bilioni kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa miundombinu chakavu, jambo likalkosaidia kuokoa umeme unaopotea na kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa umeme nchini.