Ziara ya Rais Samia China itakavyofungua fursa ya fursa

HomeKimataifa

Ziara ya Rais Samia China itakavyofungua fursa ya fursa

Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini China kufuatia mualiko alioupata kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping, inaenda kufungua milango ya fursa nyingi kwenye maeneo mbalimbali zitakazoleta maendeleo yatokanayo na mahusiano mazuri baina ya mataifa hayo mawili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na ujumbe wake kwenye mazungumzo ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping, Beijing nchini China tarehe 03, Novemba, 2022

Maeneo hayo ni pamoja na maendeleo ya miundombinu, kilimo, uwekezaji kwenye sayansi na teknolojia, biashara na kuwa na masoko ya uhakika ya kuuza bidhaa.

Rais Samia Suluhu anakuwa kiongozi wa kwanza wa nchi kutoka Afrika kuzuru China baada ya tangu kuchaguliwa tena kwa Rais Xi Jinping na pia mara yake ya kwanza kutembelea bara la Asia tangu aingie madarakani mwezi Machi mwaka 2021.

error: Content is protected !!