Fahamu taratibu za uuzaji wa bidhaa za uvuvi China

HomeKitaifa

Fahamu taratibu za uuzaji wa bidhaa za uvuvi China

China ni miongoni mwa masoko makubwa ulimwenguni yanayonunua bidhaa za uvuvi. Mkataba uliosainiwa wakati wa Ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini China, unawafungulia fursa kubwa wananchi wanaoshughulika na shughuli za uvuvi.

Bidhaa ya mabondo ya samaki inatumika sana nchini China katika utengenezaji wa supu inayotumiwa zaidi na wanawake wanaoamini kwamba unywaji wake unasaidia ngozi zao kuendelea kuwa nyororo hata wanapofikia umri mkubwa.

Mabondo hayo hutumika kama malighafi viwandani ya kutengenezea dawa inayosaidia ngozi kuwa nyororo, yanaaminika kuwa chanzo kikubwa cha protini inayosaidia ngozi kutofubaa.

Mkataba ambao Rais Dkt. Samia alishuhudia ukisainiwa umefungua fursa mpya ya uuzaji wa samaki aina ya Sangara ambao wanaaminika kuwa na madini ya Omega 3 yanayosaidia maendeleo ya ubongo.

Tangu kusainiwa kwa mkataba huo, tayari makampuni 72 yameshasajiliwa kwa ajili ya kuuza bidhaa za uvuvi katika soko la China hivyo basi Watanzania wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo kwani soko la uhakika lipo.

Taratibu za kuuza bidhaa za uvuvi kutoka Tanzania kwenda China 

-Kuwa na kampuni yenye miundombinu ya kuvua, kuchakata na kuhifadhi bidhaa za uvuvi
-Kampuni inatakiwa ijisajili katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi
-Kampuni itapewa namba ya akaunti na nywira ya kukamilisha usajili katika tovuti ya Mamlaka ya Forodha ya China (CIFE.SINGLEWINDOW.SN)
-Kampuni itapatiwa namba za usajili itakayotumiwa katika uuzaji wa bidhaa katika soko la China

Taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China imesema kama mtu binafsi anatamani kuuza bidhaa za uvuvi China, anachotakiwa kufanya ni kuvua na kuziuza kwenye kampuni ambazo zimesajiliwa na zinavibali vya kufanya biashara hiyo.

 

 

error: Content is protected !!