Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita kimeeleza kutoridhishwa na mwenendo wa usambazaji wa mbolea ya ruzuku kwa wakulima kutokana na mchakato huo kutozingatia mahitaji na msimu wa kilimo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Nicolous Kasendamila alisema hayo juzi wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano wa Kamati ya Maendeleo ya Mkoa (RCC).
Alisema chama kimefuatilia, kuhoji na kubaini kiini cha tatizo ni mawakala wa mbolea kutolipwa kwa wakati hali inayosababisha uhaba wa mbolea kwenye maeneo mengi mkoani hapo.
“Kwahiyo upande wa mbolea hatuwalaumu sana wataalamu, ni changamoto ambayo inapaswa itazamwe kwa undani zaidi,” alisema na kuongeza:
“Tumepewa taarifa mbolea imeshawasili, sasa kwa kipindi huki (Januari) Geita mbolea inakuja kufanya nini mazao yameshakomaa tayari.”