Gridi nzima ya umeme ya taifa kufumuliwa

HomeKitaifa

Gridi nzima ya umeme ya taifa kufumuliwa

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema serikali inatajaria kuanza mradi mkubwa wa kufumua gridi nzima ya umeme ya taifa na kuirekebisha.

Lengo la mradi hu ni kubadilisha miundombinu chakavu ambayo haijafanyiwa marekebisho kwa muda mrefu.

Alisema hayo bungeni jana wakati akifafanua hoja mbalimbali zilizoibuliwa wakati wa mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na kuongeza kuwa mradi huo utasainiwa Februari, mwaka huu.

January alisema mradi huo unaoitwa Gridi Imara wenye miradi 26 inayogharimu kiasi cha shilingi trilioni moja unatarajiwa kuimarisha gridi na kuifanywa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa hali itakayoondoa changamoto ya uhaba na kukatikakatika kwa umeme.

“Tuna mipango madhubuti ya kuifumua gridi ya taifa na kuirekebisha kwa sababu changamoto kubwa iliyokuwepo ni miundombinu chakavu, hili jambo ukubali ukatae ndio ukweli kwamba miundombinu yetu ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ilikuwa haitoshelezi mahitaji na haijafanyiwa marekebisho muda mrefu,” alisema Makamba.

 

error: Content is protected !!