Tanzania kinara kwa idadi ya simba dunia

HomeKitaifa

Tanzania kinara kwa idadi ya simba dunia

Waziri wa Maliasili na utalii, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza dunia kuwa na idadi kubwa ya simba zaidi ya 17,000.

Mchengerwa alitoa takwimu hizo jana jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Chama Cha Mawakala wa Utalii Wanawake Tanzania (TAWTO).

Alisema kwa mujibu wa takwimu za Taasisi ya Utalii wa Wanyamapori (TAWIRI), hadi juzi Tanzania ina simba zaidi ya 17,000 tofauti na taarifa zilizosambaa awali kuwa Tanzania ina simba 8,900.

“Idadi hii ya simba inafanya Tanzania kuwa na idadi kubwa ya simba kuliko Taifa lolote duniani na nawaomba Watanzania kuwa na wivu na nchi yetu ya Tanzania ikiwemo watoa huduma za utalii kutoa huduma nzuri na kuibua vivutio vingi vya utalii ili kufanya watalii wengi kurudi nchini,” alisema.

 

error: Content is protected !!