Fahamu mambo anayotakiwa kujua karani wa sensa

HomeKitaifa

Fahamu mambo anayotakiwa kujua karani wa sensa

Karani wa sensa atatakiwa kuuliza idadi ya watu wote waliolala katika kaya husika usiku wa kuamkia siku ya sensa. Atauliza majina ya watu wote waliolalakatika kaya hiyo usiku wa kuamkia siku ya sensa ukianzia na jina la mkuu wa kaya ambaye ni yule mtu anayewajibika kwa kaya hiyo au yule ambaye anatambuliwa na wanakaya kama kiongozi wa kaya hiyo.

Majibu ya swali hili yatawezesha kupata idadi ya watu wote nchini, wastani idadi ya watu katika kaya na kiwango cha umasikini nchini.

Swali jingine litakaloulizwa ni mtu anayehesabiwa ana uhusiano gani na mkuu wa kaya. Swali hili linalenga kujua uhusiano wa mkuu wa kaya na watu wengine kwenye kaya. Anaweza kuwa ni mke/mume wa mkuu wa kaya, mtoto wa kiume/kike, baba/mama mzazi. mjukuuu au hata ndugu.

Sensa ya watu na Makazi itafanyika Agosti 23,2022 ikiwa ni miaka kumi baada ya sensa ya mwisho iliyofanyika 2012.

error: Content is protected !!