Rais Samia aeleza mbinu za kujitosheleza kwa chakula

HomeKitaifa

Rais Samia aeleza mbinu za kujitosheleza kwa chakula

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza hatua muhimu zinazopaswa kuchukuliwa na mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuweza kujitosheleza kwa chakula kisha kuuza kwenye masoko ya ndani na nje ya jumuiya hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jana jijini Arusha, Raus Samia alisema ili kuwezesha matifa ya jumuiya hiyo kujitosheleza kwa chakula ni muhimu yakawekeza katika kilimo cha umwagiliaji.

“Ardhi pekee haitoshi, tunapanga kuangalia upatikanaji maji kwa ajili ya miradi ya umwagiliaji kwani kuna kipindi ambacho hatuna maji ya kutosha, miradi ya umwagiliaji ni mizuri kuzalisha chakula mara mbili au tatu kwa mwaka.

Pia alitoa rai kwa nchi hizo kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na reli ili mazao yanapotoka shambani yafike sokoni kwa urahisi.

“Tunatakiwa kuendelea kuwa na miundombinu bora na imara ambayo itakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi kwa kuwa mazao yakitoka shambani moja kwa oja yatakwenda sokoni kwa hara zaidi,” alisema Rais Samia.

Alisema kuna umuhimu wa nchi za EAC kuzalisha kwa wingi ili kuwa na chakula cha kutosha na kuzisaidia nchi zingine zenye uhitaji kwa kuwa kuna maeneo ya kutosha ya kilimo.

Sambamba na hilo, alisisitiza umuhimu wa kuweka akiba ya kutosha ya mbegu kwa kuzihifadhi kwenye vihenge ili ziwe kwenye usalama ambao utaleta matokeo chanya hasa kwa maeneo ya vijijini.

error: Content is protected !!