Wazo la kuhamisha Ikulu kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma lilianza mwaka 1973 ambapo Hayati Mwalimu Nyerere alitoa wazo hilo na kutaka likamilike ndani ya miaka 10 yani mwaka 1983.
Hayati Mwalimu Nyerere aliunda Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) iliyowahi kuongozwa na Mzee Pius Msekwa lakini bado uamuzi huo haukufanikiwa.
Mambo matatu yaliyokwamisha uhamuzi wa kuhamia Dodoma.
Vita dhidi ya Idi Amin
Vita dhidi ya Idi Amin ilibidi rasilimali zote za watu na pesa zikusanywe kumpiga adui.
Kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki 1977
Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika 1977 kwahiyo huduma zilizokuwa zikitolewa na Afrika Mashariki ilibidi zianze kutolewa na serikali.
Kupanda kwa bei ya mafuta duniani
Kupanda kwa bei ya mafuta duniani kulisababisha pesa za nchi za kigeni zihamie katika kuhudumia tatizo hilo.