Rais Samia anavyo-trend India

HomeKimataifa

Rais Samia anavyo-trend India

Kwenye mtandao maarufu wa Google nchini India, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekuwa mtu wa pili kwa habari zake kutafutwa sana kuliko mambo mengine yoyote.

Hili ni jambo la kuvutia kutokana na ukubwa wa India, idadi kubwa ya watu, na matumizi makubwa ya mtandao.

Ikumbukwe kuwa India ina idadi ya watu bilioni moja na milioni mia tatu, sawa na takribani mara 21 ya idadi ya Watanzania wote, na inashika nafasi ya juu kwa matumizi ya mtandao duniani. Hivyo, kuwa miongoni mwa habari zilizotafutwa sana nchini India ni jambo la jema.

Kushika nafasi ya pili kwenye orodha hiyo kunadhihirisha umaarufu wa Rais Samia Suluhu Hassan na inaweza kuonyesha maslahi ya watu wa India kuhusu shughuli na uongozi wake.

Pia, inashangaza kuona kuwa hata baada ya kifo cha mshindi wa Tuzo ya Nobel, Amartya Sen, na tangazo la kustaafu soka kwa nyota wa zamani wa Real Madrid na Chelsea, Eden Hazard, Rais Samia bado alishika nafasi ya pili kwenye utafutaji mtandaoni nchini India.

Hii inaonyesha jinsi jina lake limekuwa maarufu na linavuta umakini wa watu. Nafasi ya kwanza ikishikwa na nyota wa kriketi wa Pakistan, Babar Azam, inaonyesha jinsi mchezo wa kriketi unavyopendwa sana nchini India.

error: Content is protected !!